معلومات المواد باللغة العربية

Qasim Mafuta - Audios

Idadi ya Vipengele: 45

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Namna watu wa Maulidi walivyo waelewa vibaya wana chuoni na kuwasingizia uongo.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Uzushi wa kusherehekea Maulidi umenzishwa mwanzoni mwa karne ya sita.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Maulidi ni Bidaa dhwalaalah (Uzushi na upotovu), pia imeelezea namna wazushi wasivyo na hoja na wanafuata matamamnio ya nafsi zao.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Nini maana ya Bidaa ( Uzushi ) kilugha na kisheria, pia imeelezea hatari ya Uzushi.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Kwa mujibu wa Uislamu pamoja na mahji ya Ahlu Sunna wal Jamaa, Kusherehekea Maulidi hayakuwepo na ni Uzushi.

  • Kiswahili

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    1- Mada hii inazungumzia: Zama za fitna na kwamba nilazima watu wachukue tahadhari, pia imezungumzia umuhimu wa kutafuta elim yenye manhji ya kufuata sunna za Mtume (s.a.w). 2- Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa muislam madhubuti katika imani yake, pia imezungumzia hatari ya kufuata au kufanya jambo bila ya elim, nakwamba nisababu ya kuingia katika fitna.

  • Kiswahili

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    Mada hii inazungumzia: Uzushi wa Shahada ya tatu katika Adhana ya Mashia, nakwamba hakuna hata riwaya dhaifu inayo thibitisha shahada hiyo.

  • Kiswahili

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    Mada hii inafafanua: Namna ya kufanya kwa mtu anaetaka kuacha Ushia, pia inafanua mambo mbalimbali kuhusu mashia na itikadi mbovu walizonazo.

  • Kiswahili

    Anuwani ya mada hii ni Misingi ya da’awa ya kweli, pia inazungumzia: Umuhimu wa elimu na maoni ya watu katika kutengeneza umma wa kiislam.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Daraja za jihadi, ni wakati gani jihadi inakuwa ni lazima, vievile inazungumzia maneno ya wanachuoni kuhusu jihadi.

  • Kiswahili

    Anuwani ya mada hii ni: Hijabu ya kisheria na Nasaha kwa wanawake.shekh amezungumzia Sharti za Hijabu,na umuhimu wa kushikamana na dini kwa wakina mama.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia msimamo wa Uislam kuhusu kuhusu kupigana Jihadi katika njia ya Allah, na upambanuzi wake, na tatizo la waislam wengi kuto fatilia mambo kwa kina, na madhara ya Hamasa.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia aina za jihadi,akasema shekh kuwa jihadi ina aina mbili :Jihadiya kujitetea, na Jihadi ya ilio tangazwa na Kiongozi.

  • Kiswahili

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    1- Mada hii inazungumzia: Maana ya Hijja kilugha na kisheria, na ni nguzo katika nguzo tano za uislam, pia imebainisha kwamba Hijja ni fardhi inatekelezwa mara moja katika umri. 2- Mada hii inazungumzia: Umuhimu kwa mwenye kuhiji kuwa na nia thabiti pamoja na kujikurubisha kwa Allah, pia imezungumzia mambo ya kujifunza katika ibada ya Hijja na tahadhari ya kuiga uzushi. 3- Mada hii inazungumzia: Hijja na Umra na fadhila zake pamoja na alama za mwenye kufanya Hijja ya kweli, pia imezungumzia kwamba Hijja ni fardhi kwa waislam wote wanaume na wanawake. 4- Mada hii inazungumzia: Aina za maandalizi ya Hijja na imefafanua kuhusu Hijja ya mtoto mdogo, pia imezungumzia umuhimu wa kuchunga utaratibu na makatazo baada ya Ihram. 5- Mada hii inazungumzia: Namna Mtume (s.a.w) alivyoruhusu kumuhijia mzazi asiyejiweza kutokana na uzee au ugonjwa, na kwamba inafaa mwanaume kumuhijia mwanamke na mwanamke kumuhijia mwanaume, pia mada hii ina maswali na majibu.

  • Kiswahili

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    1- Mada hii inazungumzia: Ubora wa mtu kuwa mkeli, na kwamba ukweli ni katika sharti za laa Ilaha ila Lllah, na ukweli ni utulivu wa nafsi bali uongo ni mashaka, pia imezungumzia umuhimu wa kufanya mambo kwa ajili ya Allah. 2- Mada hii inazungumzia: Alama za watu wakweli, kama vile utulivu wa moyo, na kuipa nyongo dunia na kujiepusha na riyaa, na anaeshikamana na Sunna wakati wa fitna, pia amezungumzia maana ya zuhdi. 3- Mada hii inazungumzia: Alama za ukweli nikuficha matendo mema, na kuhisi upungufu katika matendo yake, nakuyafanyia umuhimu na dini yake, na anathibiti kwenye dini wakati wa fitna, na kuikubali haki na kujisalimisha kwenye haki

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia Siku ya Arafa, ubora wake, nakwamba Allah anashuka na kuwasogelea kwa waliosimama katika viwanja vya Arafa, na Allah anajifakhari kwa malaika, na yanayo takiwa kufanywa nawale ambao hawako katika viwanja vya Arafa.

  • Kiswahili

    1- Mada hii inazungumzia Siku ya Arafa, maana yake na umuhimu wa kuomba dua katika siku hiyo, na amejibu kuhusu utata juu ya siku ya arafa na siku ya Iddi al Adhha nawale wasiofunga siku ya arafa bali wanafunga siku ya kuchinja. 2- Mada hii inazungumzia Majibu ya utata wa Arafa na hijja, amebainisha kuwa hija ilikuwepo tangu wakati wa nabii Ibrahim haikuwa faradhi, amefafanua mafungaamano ya Arafa na mwezi Dhulhijah, na Arafa ya mtu wa China na Est Africa, na mafungamano ya swala ya iddi na kupiga mawe na kuchinja kwa mahojaji . 3- Mada hii inazungumzia Majibu ya utata wa Arafa na hijja, amebainisha kuwa watu wanafuata mahujaji katika takbira, na kuchinja ili wafuate watu wa mina, na ametaja Qauli za wanachuoni kuhusu mafungamano ya hija na matendo ya wasiokuwa mahujaji.

  • Kiswahili

    1- Khutuba ya Iddi amezungumzia neema ya kuwa na uongofu nakufikishwa katika mwezi wa Ramadhan, na wepesi wa kumalizika umri, na kwamba Ramadhani nishule, na malengo ya swaumu niuchamungu, na kulifikia lengo hilo nikufanya mema baada ya Ramadhani. 2- Khutuba ya Iddi amezungumzia sababu za kufuata makundi yalio potea na fikra potovu nikuto kuisoma elimu ya dini, na kukosa malezi bora kwa mtoto, na wazazi kuwatupa watoto wao, Na kuinusuru dini nikuisoma dini, pia ametaja adabu za Iddi

  • Kiswahili

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    Mada hii inazungumzia: Mambo yanayoifanya swaumu iwe sahihi na yanayoifanya swaumu kuwa si sahihi, pia imezungumzia umuhimu wa kujiepusha na uongo, kusengenya, na dhulma na vikao vya kipuuzi ndani ya mwezi wa Ramadhani.

  • Kiswahili

    Mhadhiri : Qasim Mafuta Kurejea : Yunus Kanuni Ngenda

    Mada hii inazungumzia: Namna mwadamu alivyojisahau katika duania, na kusahau kwamba ipo siku atatolewa roho yake, imezunguzia sifa za waja wema walio faulu duniani na akhera