معلومات المواد باللغة العربية

Abubakari Shabani Rukonkwa - Audios

Idadi ya Vipengele: 97

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Namna watu wa Maulidi walivyo waelewa vibaya wana chuoni na kuwasingizia uongo.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Uzushi wa kusherehekea Maulidi umenzishwa mwanzoni mwa karne ya sita.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Maulidi ni Bidaa dhwalaalah (Uzushi na upotovu), pia imeelezea namna wazushi wasivyo na hoja na wanafuata matamamnio ya nafsi zao.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Nini maana ya Bidaa ( Uzushi ) kilugha na kisheria, pia imeelezea hatari ya Uzushi.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Kwa mujibu wa Uislamu pamoja na mahji ya Ahlu Sunna wal Jamaa, Kusherehekea Maulidi hayakuwepo na ni Uzushi.

  • Kiswahili

    Mada hii inakamilisha mada iliyo pita inaelezea msiba wa kuishi mwanamume na mwanamke bila kufunga ndoa, kisha ameeleza ubora wa kutafuta elimu.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia ubora wa masiku kumi ya dhil hija kisha ameeleza kuwa Elimu ndio kibainisho cha halali na haramu na ndio sababu ya kumuabudu Allah kwa usahihi, na mtu asie kuwa na elimu ya dini anakuwa kama mfu.

  • Kiswahili

    1- Mada hii inazungumzia: Uzito wa dhambi ya uzinifu na kwamba ni katika madhambi makubwa yenye kuangamiza, pia imezungumzia makatazo ya Allah juu ya uchafu wa zinaa na kuto kuikaribia zinaa, pia amezungumzia nyumba za zinaa. 2- Mada hii inazungumzia: sifa za watu wema na adhabu za wazinifu, kisha amebainisha madhambi makubwa, kisha akataja kuwa kuikurubia zinaa niharamu na nitabia mbaya. 3- Mada hii inazungumzia: Sababu za uzinifu miongoni mwa sababu hizo nikuviachia viungo na kuto kuweka mipaka katika kuishi na wanawake, nakuto kuinamisha macho na ndimi, sababu ya pili nikuzurura na wanawake na kuongozana nao. 4- Mada hii inazungumzia: Dhambi za uzinifu na sababu zake sababu ya tatu nikupeyana mikono na kugusana, na amezungumza uzito wa dhambi ya kumshika mwanamke asie halali kwake, pia ametaja sababu zinazo pekelea kugusana, sababu ya nne nikuingia katika sehemu za wanawake. 5- Mada hii inazungumzia: Sababu za uzinifu miongoni mwa sababu hizo ya tano nikukaa faragha mwanamume na mke ila akiwa nimahrim, katika faragha nikurejea masomo wanawake na wanaume katika vyuo na mashule, na katika kuchumbiyana, kisha amezungumza uwezo wa mwanamke katika kumpa mtihani mwanamume.

  • Kiswahili

    • Mada hii inazungumzia: Haki za binadamu katika uislam amezungumzia maana ya haki na umuhimu wa kujuwa haki za binadamu na ulazima wa kuzilinda, pia ametaja haki tano katika Quraan kwa ujumla. • Mda hii inazungumzia: maana ya binadamu na maana ya uislam, na ametaja mafundisho ya uislam kuhusu haki za binadamu. • Amezungumza kuwa uislam ndio wakwanza kufundisha haki za binadam, Haki ya kwanza (Haki ya kuishi). • Mada hii inazungumzia: Uharam wa kujiua na niharam kutumia kitu ambacho kitamsababishia kifo, kama kuvuta sigara na pombe nk, pia amezungumzia haki ya pili (Kulinda mali za watu) na uharam wa kudhulumiana. • Mada hii inazungumzia: Uharam wa kudhulumiana na chanzo chake, pia amezungumzia uharam wa kula riba na njama za nchi zilizo endelea katika kula riba, pia kazungumzia uharam wa kula rushwa, na dhulma nimaradhi yanayo ambukiza. • Mada hii inazungumzia: Haki za binadamu ikiwemo mwanamke kuheshimiwa utu wake, amebainisha hali ya mwanamke kabla ya uislam, na jinsi uislam ulivyo linda heshima ya mwanamke, kabainisha jinsi mwanamke anavyo dhalilisha mwanamke katika karne ya 21. • Mada hii inazungumzia: Haki za binadamu ikiwemo haki ya kuabudu, na amebainisha kuwa hakuna kulazimishana, kasha akataja hali ya ulinganiaji wakati wa mtume na uongo wa wale wanao sema uislam ulienezwa kwa upanga, bali uislam uliingia kwa hoja zenye nguvu. • Mada hii inazungumzia: Haki za binadamu nayo nihaki ya mwanadamu kuwa huru, na msingi wa uhuru wa binadamu, ambayo inatolewa katika maneno ya Omar bin Khatwabi (r.a).

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia:Fadhila za kutawadha, ikiwemo kuwa na Nuru kwa mwenye kutawadha, pia miongoni mwa ubora wa Udhu nikufutiwa madhambi yake.na kwamba udhu ni silaha kwa Muumini.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kufanya bidii katika kutafuta elimu, na kuutumia wakati katika kujisomea fani tofauti, na kuto tosheka na masomo ya darasani.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Mambo mawili yanayomkinga mwanadam na adhabu za Allah, na imezungumzia pia masharti ya toba.

  • Kiswahili

    Anuwani ya mada hii ni Misingi ya da’awa ya kweli, pia inazungumzia: Umuhimu wa elimu na maoni ya watu katika kutengeneza umma wa kiislam.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Daraja za jihadi, ni wakati gani jihadi inakuwa ni lazima, vievile inazungumzia maneno ya wanachuoni kuhusu jihadi.

  • Kiswahili

    Anuwani ya mada hii ni: Hijabu ya kisheria na Nasaha kwa wanawake.shekh amezungumzia Sharti za Hijabu,na umuhimu wa kushikamana na dini kwa wakina mama.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia msimamo wa Uislam kuhusu kuhusu kupigana Jihadi katika njia ya Allah, na upambanuzi wake, na tatizo la waislam wengi kuto fatilia mambo kwa kina, na madhara ya Hamasa.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia aina za jihadi,akasema shekh kuwa jihadi ina aina mbili :Jihadiya kujitetea, na Jihadi ya ilio tangazwa na Kiongozi.

  • Kiswahili

    Maana ya Aibu pila ameeleza kua Allah anazijua siri zetu, kisha ameeleza udhaifu wa mwanadamu na tabia za watu katika kusema aibu za wenzao, na tiba ya maradhi ya kutangaza aibu za watu.

  • Kiswahili

    Mada hii inaelezea nafasi ya nia katika ibada, ameeleza maana ya nia na mahala pake katika ibada na jinsi ya uweka nia katika ibada.

  • Kiswahili

    Mada hii inaelezea hatuwa za kufanya katika kutibu maradhi ya Umbeya, na katika hatuwa hizo ni kuthibitisha habari unazo zipata, kisha akaeleza kuwa waganga wa kienyeji(Washirikina) na wachawi nikatika wanao ongoza kwa kusengenyaji(Umbeya).