معلومات المواد باللغة العربية

Abubakari Shabani Rukonkwa - Audios

Idadi ya Vipengele: 97

  • Kiswahili

    Mada hii inaelezea: Maana ya kusengenya (Umbeya) na kwamba ni katika madhambi makubwa, kisha amebainisha sifa za watu wenye umbeya, na kwamba nimtu washari, na ataadhibiwa katika kaburi lake.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia Maada ya pombe na hukumu ya kutumia na kuuza pombe, kisha amebainisha kuwa madawa ya kulevya ni katika yana hukumu ya pombe, na ameelezea madhara ya madawa ya kulevya kiafya kidini na kijamii na kwamba pombe ni mama wa Machafu.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia sababu za kupata mali, miongoni mwa sababu hizo: Ni Uchamungu, na ukweli katika maneno na vitendo na katika niya yake, hiyo nisababu ya kutengamaa mambo yote.

  • Kiswahili

    Mada inazungumzia Miongoni mwa kuihesabu nafsi nikutekeleza ibada ya swala, na familia yote, na kwamba swala ndio funguo za rizki, kisha ameeleza hali ya watu na swala zao pindi wanapo safiri zao, pia ameleza umuhimu wa kuhesabu mali ili kuzitolea zaka.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia miongoni mwa kuihesabu nafsi ni kuihesab nafsi na kujuwa chanzo cha uovu wake, na kwanini inapata uzito wa kuswali! Kisha amezungumzia umuhimu wa kujuwa uhalali na uharamu wa vyakula vyetu, na kwamba mtu asie swali nikafiri.

  • Kiswahili

    Mada hii imezungumzia ufupi wa umri wa mwanadamu, nakwamba ameumbwa kutokana na masiku, kisha akabainisha kuwa katika kuihesabu nafsi nikujuwa mema aliyo yafanya, na kwamba kuikaguwa nafsi nikatika alama ya Uchamungu.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia Umuhimu wa kuwa mchamungu na hasara za kukosa uchamungu kisha akaelezea kuwa Mwaka mpya nimwaka wa kuihesabu Nafsi.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia:miongoni mwa matendo mema katika masiku kumi ya mfungo tatu, na amebainisha ubora wa kutowa salam, Kuunga udugu na kuwafanyia wema wazazi, na kuchunga haki za mume na mke.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: umuhimu wa kufunga siku ya arafa, na mambo anayo takiwa afanye katika masiku kumi ya mfungo tatu.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Fursa ya kuyafikiwa na masiku bora duniani, kisha ametaja miezi mitukufu, na akaeleza ubora wa masiku hayo, na ubora wa siku ya Arafa.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa Uchamungu, na maana ya khutbatu Alhaja, kisha akabainisha swala ya khusufu na Malengo ya khusufu.

  • Kiswahili

    Mada hii inakamilisha mada iliyo pita imeelezea hali za watu wamotoni na vyakula vyao na nguo zao, pia mezungumzia maneno ya shetani atakayo zungumza motoni.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia khutba ya mkosi na sababu ya kuitwa hivyo pia amezungumzia vitisho vya siku ya Qiyama.

  • Kiswahili

    Silsila ya mada za sauti za Tarjama ya Quran tukufu kwa lugha ya kiswahili inayo itwa "Al Muntakhab Fi Tafsir Al Qur’an" iliyo fanywa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani tafsiri hii inasifika kwa ufasaha wa lugha, masahafu huu umekusanya sauti ya msomaji wa Quraan, na sauti ya anaesoma tarjama ya kiswahili.

  • Kiswahili

    1- Mada hii inazungumzia: Baadhi ya sababu za Muislam kuharakisha kuitekeleza ibada na nguzo ya Hajji, yakwanza nikuharakia kutumia nafasi ya kuwa na uwezo, sababu ya poli nikwamba hujuwi utakufa lini, pia amezungumzia sababu batili wanazo towa wasio taka kuhiji. 2- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za muislam kuharakisha ibada ya Hijja ni umuhimu na ubora wa ibada hiyo, pia imezungumzia umuhimu kwa muislam kukimbilia jambo la kheri 3- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za muislam kuharakisha ibada ya Hijja ni kwamba Hijja ni sababu ya kusamehewa madhambi yote, pia imezungumzia umuhimu wa kuchunga na kuhifadhi matendo ya Hijja 4- Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za muislam kuharakisha ibada ya Hijja ni kwamba malipo ya Allah kwa mtu aliyefanya ibada ya Hijja ni Pepo, pia imezungumzia ubora wa neema ya Pepo ya Allah.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia Ufalme wa Allah na kwamba anachukia pindi unapo acha kumuomba, na nahakika mwanadamu anapo ombwa anachukia, na anampa kila mwenye kumuomba na Allah ndio mmiliki wa mbingu na ardhi.

  • Kiswahili

    1- Mada hii inazungumzia: makatazo ya kuudhiana waislam na kwamba wanao muudhi Allah na Mtume wake (s.a.w) wana laana kubwa, pia imezungumzia aina mbili za maudhi ambayo ni maudhi ya maneno na vitendo. 2- Mada hii inazungumzia: Hatari ya madhambi na maudhi ya kusengenya na kwamba hao ndio wanaokula nyama za watu, pia imezungumzia maudhi ya vitendo kama vile kumuudhi jirani kwa kutumia vyombo vya kileo na kutia uchafu katika katika njia.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia saa ya kujibiwa dua ambayo inapatikana siku ya ijumaa, amebainisha wakati huo, na pindi mtu anaposhtuka usingizini akiwa amelala na udhu, na baina ya Adhuhuri na Asri siku ya ijuma tano

  • Kiswahili

    1- Mada hii inazungumzia umuhimu wa kuandaa darsa kwa wanawake, kwasababu ndio wengi motoni, na ametaja sababu za kuwa wengi motoni, kasha amehusiya watu wahifadhi ndimi zao. 2- Mada hii inazungumzia sababu ya wanawake kuingia motoni kama kulani sana na kukataa wema wa mume wake, ametaja jinsi mwaname anavyo shawishika katika zama hizi, kisha amezungumzia maana ya ugeni katika dini . 3- Mada hii inazungumzia baadhi ya mifano kwa wanawake walio pata mateso lakini wakathibiti katika dini, kama Mwanamke aliekuwa anafanya kazi ya kuwasuka mabinti wa Firauni, na mke wa Firauni amehimiza umuhimu wa kuithamini Dini. 4- Mada hii inazungumzi halia za wanawake wa kiislam na udhaifu wao katika ibada nakudai kwao haki sawa, na baadhi ya hoja dhaifu katika kuvaa hijabu, kisha akabainisha umuhimu wa mwanamke wa kiislam kushikamana na dini. 5- Mada hii inazungumzia tabia ya kusengenya wanawake, na uharamu wake, na uwajibu wa kuhifadhi ndimi, kisha akataja kuwa mwanamke atakaeshikamana na dini atakuwa peponi na familia yake.

  • Kiswahili

    Mada hii inazungumzia Siku ya Arafa, ubora wake, nakwamba Allah anashuka na kuwasogelea kwa waliosimama katika viwanja vya Arafa, na Allah anajifakhari kwa malaika, na yanayo takiwa kufanywa nawale ambao hawako katika viwanja vya Arafa.